UPENDO WA KWELI


UPENDO WA KWELI
Katika maisha yangu ya imani na miito, ni vyema kujikumbusha na kuelewa kwamba ‘Mungu ananijua zaidi ya ninavyo jijua mimi’ na pia “Mungu ananipenda zaidi ya ninavyo jipenda mimi”. Ananijua na ananipenda, kwahiyo ni jukumu na wajibu wangu mimi kama kijana kuwa mtu wa KUMWAMINI.
            Kuna mambo makuu matatu ambayo ni  ya msingi saaana mimi kama kijana yanipasa kuyashiriki na kuyaishi. Kuyatambua mambo haya tujiiulize maswali kwa  uaminifu; Moja,  je, nipo katika hali ya neema?- Kuishi maisha ya neema ni kule kuwa katika namna ambayo ni ya kumpendeza Mungu; Hali ya kuishi maisha ya usafi wa moyo, kuyapenda masakramenti ya kanisa, kujitoa kwa ajili ya wale wasiojiweza hasa masikini , wagonjwa na wote walio katika mazingira magumu, kulipenda na kuliishi neno la Mungu, kuishi maisha yasio ya pande mbili, kuyapenda mambo ya kiroho na pia kuwa katika hali ambayo sio ya dhambi. Hii ndio hali ya neema hali ambayo yampasa kijana kijana yeyote aiishi, mimi nitajivunia na kutambua kwamba naiishi hali ya neema pale ninapoishi maisha ya kumpenda Mungu na jirani yangu.  Swali la pili kujiuliza ni kwamba Je, natimiza wajibu wangu wa kila siku?, kulingana na rika letu na shughuli zangu za kila siku , ikiwa mimi ni mawanafunzi ninalazimika kusoma kwa bidii na kutumia vyema mda wangu ili niweze kufanikiwa katika masomo yangu. Cha kwanza kwanza,wajibu wangu wa kwanza kama mwanafunzi ni kusoma kwahiyo nilazima mimi kuyatanguliza masomo yangu mbele ya vyote, kama nimfanyakazi lazima kuithamini kazi yangu na kuipenda. Sisi kama vijana ni tunakumbushwa kwamba ni wajibu wetu kuyatunza mazingira, kusaidia wanafamilia, kuwasahihisha wanaoenda kinyume cha maadili, kutenda yaliyo mema siku zote. Mimi kama kijana ni wajibu wangu kuutumia vyema uhuru
niliojaliwa na mwenyezi Mungu kwa kuisha kwa maadili na kwa kumcha Mungu, niitumie vyema teknologia, simu yangu isiniongoze bali niiongoze mimi, nitambue mimi kama kijana kila kitu kina muda wake katika maisha na pia kukataa kudanganyika. Swali la tatu mimi kama kijana linalonipasa kujiuliza ni  je, nilisali leo? Kati ya mambo ya msingi ambayo kijana mcha Mungu hanabudi kuyafuata ni kuwa mtu wa sala. Mtu wa sana ni yule siku zote hutafakari na huwa na fikra zilizo njema anayetambua mapungufu yake na kumrudia Mungu, anayependa na kulifuata neno la Mungu, anaye shiriki masakramenti ya kanisa na anayezungumza na Mungu na kumkabithi maisha yake ayatawale. Sala ni silaha ya pekee thidi ya muovu shetani, kujana anayependa maisha ya sala huwa na moyo wa kutafakari juu ya maisha yake na kufanya chaguzi zilizo jema juu ya maisha yake.
Mimi kama nisipokuwa katika hali ya Neema, nisipo fanya yale ninayopaswa kufanya, nisipo timiza wajibu wangu wa kila siku ni sawa na kusema Hapana kwa Mungu. Mimi kama kijana nijiwekee ratiba yangu ambayo nahitaji kuifuata, ni kipi nikifanye ili niweze kuwa katika hali ya neema, kama sisali yanipasa nianze kusali, muda wangu ninaoupoteza kwenye mitandao ya kijamii kutuma na kupekua maambo yasiyo faa, yaniapasa kuacha. Pambano bila upinzani halifurahishi tujiwekee mipaka katika maisha yetu ili tuweze kuyafurahia maisha yenye fanaka mbeleni. Wakusoma wasome kwa bidii zote na wakufanya kazi wafanye kwa uaminifu na kwa nguvu zao ili waweze kuvuna kadiri wapandavyo. Tukumbuke Mungu akiwa katikati ya shughuli zangu hakika hakuna kitakachoshindikana. Ni wajibu wangu kusema kweli ndani ya moyo wangu, kama ninaumwa sikio langu ni lazima nimwambie dactari ukweli kuhusu sikio langu ili niweze kupata matibabu mazuri. Tusijidanganye tuseme kweli na tutasimama imara katika hii safari ya kutambua miito yete.

Comments